Ruka hadi kwa yaliyomo kuu

Mipangilio ya kuki

Tunatumia vidakuzi ili kuhakikisha utendakazi msingi wa tovuti na kuboresha matumizi yako ya mtandaoni. Unaweza kusanidi na kukubali matumizi ya vidakuzi, na kurekebisha chaguo zako za idhini, wakati wowote.

Muhimu

Mapendeleo

Uchanganuzi na takwimu

Masoko

Je, unahitaji kuongeza malalamiko? - wasiliana nasi sasa!

6 Machapisho

Asante kwa kutushirikisha changamoto unazopitia katika ufugaji wa kuku ๐Ÿ”
Changamoto ambazo zimetajwa mara nyingi ni uhaba wa chakula cha kuku ๐Ÿฝ๏ธ, bei kubwa za chakula cha kuku ๐Ÿ’ธ, uhaba na gharama kubwa za dawa za kuku ๐Ÿ’Š na chanjo ๐Ÿ’‰, pia magonjwa ๐Ÿค’, vifo na ukosefu wa masoko ๐Ÿ›’.
Upungufu wa vitamini (avitaminosis)
Upungufu wa vitamini (avitaminosis) kwa kuku hutokea wakati vitamini muhimu hazipatikani katika mlo ๐Ÿฅฆ. Huathiri kuku wa rika zote ๐Ÿฅ. Dalili: Macho yenye mawingu ๐Ÿ‘€, kudumaa, kuhara ๐Ÿ’ฉ, kukonda, vidole vilivyojikunja, ulimi uliovimba ๐Ÿ‘…, ganda kuzunguka mdomo na macho, na kupooza kwa miguu ๐Ÿšซ. Matibabu: Tumia vitamini sahihi ๐Ÿ’Š na wasiliana na daktari wa mifugo ๐Ÿ‘ฉโ€โš•๏ธ. Kinga: Wape kuku mboga mbichi mara kwa mara ๐ŸŒฑ, ongeza vitamini kwenye chakula na maji, na utumie virutubisho vya wanyama.
MAHITAJI YA CHAKULA CHA SIKU KWA KUKU 100 ๐Ÿ”
๐Ÿ“… 0 - 8 wiki = ๐Ÿฃ 6 kg za chakula cha vifaranga ๐Ÿ“… 9 โ€“ 16 wiki = ๐Ÿฅ 9 kg za chakula cha wanaokua ๐Ÿ“… 17 - 19 wiki = ๐Ÿ“ 10-11 kg za chakula cha wanaojiandaa kutaga ๐Ÿ“… 20 wiki na kuendelea = ๐Ÿฅš 12-13 kg za chakula cha kuku wanaotaga โš ๏ธ Angalizo: Ni muhimu kufuata ratiba ya ulishaji wa kuku wako kwa usahihi ili uweze kuepuka kulisha kuku wako kwa hasara. ๐Ÿ“Œ Ratiba hii ni kwa kuku chotara na wa mayai tu.
๐Ÿ’‰๐Ÿ“RATIBA YA UTOAJI WA CHANJO KWA KUKU WA CHOTARA NA MAYAI
SIKU YA 7 ๐Ÿ—“๏ธ Wapatie kuku wako chanjo ya Mdondo, Magwa Newcastle Vaccine SIKU YA 14 ๐Ÿ—“๏ธ Wapatie kuku wako chanjo ya Gomboro, IBD Gomboro Vaccine SIKU YA 21 ๐Ÿ”„ Rudia chanjo ya Mdondo, Magwa Newcastle Vaccine SIKU YA 28 ๐Ÿ”„ Rudia chanjo ya Gomboro, IBD Vaccine SIKU YA 35 ๐Ÿ—“๏ธ Wachome kuku wako chanjo ya Ndui, Fowl Pox Vaccine โš ๏ธ๐Ÿฆ  MUHIMU: Zingatia ushauri wa matumizi sahihi kwa kila chanjo pindi uinunueโœ…
CHANJO
๐Ÿ“๐Ÿ’‰Kumbuka utumiaji wa chanjo ni muhimu mno ili kukinga kuku wako dhidi ya magonjwa nyemelezi kama vile Mdondo, magwa na ndui. ๐Ÿ‘ฉ๐Ÿพโ€โš•๏ธZingatia maelezo kutoka kwa mtaalamu kabla ya matumizi ya chanjo. โš ๏ธMambo muhimu ya kuzingatia ni kama yafuatayo 1๏ธโƒฃ ๐Ÿšซ๐Ÿฆ  Hakikisha unapotoa chanjo kuku wako hawana maambukizi ya maradhi 2๏ธโƒฃ ๐ŸฃZingatia umri wa kuku wako kabla ya kutoa chanjo
KONGAMANO LA UMUHIMU WA MIKATABA YA KIBIASHARA
๐Ÿค๐Ÿ’ตKongamano lilijumisha wadau wa ufugaji wa kuku wa kisasa na wanunuzi. ๐Ÿ“โ€ผ๏ธLengo la kongamano hili ni kutoa uelewa juu wa umuhimu wa mikataba rasmi katika biashara za bidhaa wanazozalisha wafugaji kama vile mayai ๐Ÿฅšna kuku๐Ÿ“. โš–๏ธMiongoni mwa mada zilizojadiliwa kwenye kongamano ni aina za mikataba inayotambulika kisheria. โœ…โœ๏ธBaada ya mafunzo wafugaji walitekeleza mafunzo kwa kuingia kwenye mikataba ya kimaandishi.

Thibitisha

Tafadhali ingia

Nenosiri ni fupi mno.

Shiriki