Ruka hadi kwa yaliyomo kuu

Mipangilio ya kuki

Tunatumia vidakuzi ili kuhakikisha utendakazi msingi wa tovuti na kuboresha matumizi yako ya mtandaoni. Unaweza kusanidi na kukubali matumizi ya vidakuzi, na kurekebisha chaguo zako za idhini, wakati wowote.

Muhimu

Mapendeleo

Uchanganuzi na takwimu

Masoko

Je, unahitaji kuongeza malalamiko? - wasiliana nasi sasa!

8 Machapisho

Shukrani kwa washiriki wa5 waliotoa maoni namna gani NCA inaweza kuwasaidia wafugaji wa kuku.
Wamekubali kuwa NCA inaweza kusaidia wafugaji mafunzo ya ya vitendo juu ya ufugaji bora,matumizi sahihi ya dawa na chanjo na juu ya kuongeza idadi ya kuku. Wengi pia wamegusia uhutaji wa mitaji, pembejeo na fursa za masoko kukuza ufugaji wa biashara
Mipango ya 2026
NCA inakusudia kutoa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku, matumizi sahihi ya chanjo na dawa. Halikadhalika,tunaendelea kutafiti njia rahisi za upatikanaji wa vifaranga na chakula cha kuku.
Asante kwa kutushirikisha changamoto unazopitia katika ufugaji wa kuku 🐔
Changamoto ambazo zimetajwa mara nyingi ni uhaba wa chakula cha kuku 🍽️, bei kubwa za chakula cha kuku 💸, uhaba na gharama kubwa za dawa za kuku 💊 na chanjo 💉, pia magonjwa 🤒, vifo na ukosefu wa masoko 🛒.
Upungufu wa vitamini (avitaminosis)
Upungufu wa vitamini (avitaminosis) kwa kuku hutokea wakati vitamini muhimu hazipatikani katika mlo 🥦. Huathiri kuku wa rika zote 🐥. Dalili: Macho yenye mawingu 👀, kudumaa, kuhara 💩, kukonda, vidole vilivyojikunja, ulimi uliovimba 👅, ganda kuzunguka mdomo na macho, na kupooza kwa miguu 🚫. Matibabu: Tumia vitamini sahihi 💊 na wasiliana na daktari wa mifugo 👩‍⚕️. Kinga: Wape kuku mboga mbichi mara kwa mara 🌱, ongeza vitamini kwenye chakula na maji, na utumie virutubisho vya wanyama.
MAHITAJI YA CHAKULA CHA SIKU KWA KUKU 100 🐔
📅 0 - 8 wiki = 🐣 6 kg za chakula cha vifaranga 📅 9 – 16 wiki = 🐥 9 kg za chakula cha wanaokua 📅 17 - 19 wiki = 🐓 10-11 kg za chakula cha wanaojiandaa kutaga 📅 20 wiki na kuendelea = 🥚 12-13 kg za chakula cha kuku wanaotaga ⚠️ Angalizo: Ni muhimu kufuata ratiba ya ulishaji wa kuku wako kwa usahihi ili uweze kuepuka kulisha kuku wako kwa hasara. 📌 Ratiba hii ni kwa kuku chotara na wa mayai tu.
💉🐓RATIBA YA UTOAJI WA CHANJO KWA KUKU WA CHOTARA NA MAYAI
SIKU YA 7 🗓️ Wapatie kuku wako chanjo ya Mdondo, Magwa Newcastle Vaccine SIKU YA 14 🗓️ Wapatie kuku wako chanjo ya Gomboro, IBD Gomboro Vaccine SIKU YA 21 🔄 Rudia chanjo ya Mdondo, Magwa Newcastle Vaccine SIKU YA 28 🔄 Rudia chanjo ya Gomboro, IBD Vaccine SIKU YA 35 🗓️ Wachome kuku wako chanjo ya Ndui, Fowl Pox Vaccine ⚠️🦠 MUHIMU: Zingatia ushauri wa matumizi sahihi kwa kila chanjo pindi uinunue✅
CHANJO
🐓💉Kumbuka utumiaji wa chanjo ni muhimu mno ili kukinga kuku wako dhidi ya magonjwa nyemelezi kama vile Mdondo, magwa na ndui. 👩🏾‍⚕️Zingatia maelezo kutoka kwa mtaalamu kabla ya matumizi ya chanjo. ⚠️Mambo muhimu ya kuzingatia ni kama yafuatayo 1️⃣ 🚫🦠 Hakikisha unapotoa chanjo kuku wako hawana maambukizi ya maradhi 2️⃣ 🐣Zingatia umri wa kuku wako kabla ya kutoa chanjo
KONGAMANO LA UMUHIMU WA MIKATABA YA KIBIASHARA
🤝💵Kongamano lilijumisha wadau wa ufugaji wa kuku wa kisasa na wanunuzi. 📝‼️Lengo la kongamano hili ni kutoa uelewa juu wa umuhimu wa mikataba rasmi katika biashara za bidhaa wanazozalisha wafugaji kama vile mayai 🥚na kuku🐓. ⚖️Miongoni mwa mada zilizojadiliwa kwenye kongamano ni aina za mikataba inayotambulika kisheria. ✅✍️Baada ya mafunzo wafugaji walitekeleza mafunzo kwa kuingia kwenye mikataba ya kimaandishi.

Thibitisha

Tafadhali ingia

Nenosiri ni fupi mno.

Shiriki